Unaweza ukawa unajiuliza, ni vipi sasa kompyuta inafanya kazi kama ina sakiti ambazo
zinaweza kufikia milioni kumi? Je si kifaa kilicho tata sana?
Kwa ujumla kompyuta haifanyi kazi vigumu kiasi hicho kama unavyoweza kudhani.
Sakiti hizo zinaisaidia kufanya kazi nyingi kwa wakati mmoja na kwa haraka sana na
ndiyo matarajio ya binadamu; kwamba ifanye kazi kwa haraka sana ili kufanya uzalishaji mali
kuwa mkubwa. Maelekezo ambayo kompyuta inatoa na kufanya (baada ya kupewa na binadamu)
ni rahisi kabisa: jumlisha namba moja na nyingine, toa data kutoka sehemu moja kupeleka sehemu
nyingine, peleka habari kutoka kifaa kimoja kwenda kifaa kingine, punguza jotoridi la kifaa fulani
endapo jotoridi hilo litazidi kiwango kilichowekwa na kadhalika. Maelekezo haya hufanyika Kwa
haraka Sana kiasi kwamba unapata majibu unayoyataka papo kea papo!
Ni jambo moja tu ambalo linaifanya kompyuta kuwa tofauti Na mashine nyingine katika dunia hii:
jambo hili Ni kwamba kompyuta inaweza kupangiliwa kufanya mambo kutokana na matakwa ya
mtumiaji (can be programmed). Hii inamaanisha kuwa mpangilio wa maelekezo (a list of
instructions) ambayo ndiyo huitwa programu ya kompyuta (computer program) huweza kuingizwa
katika kompyuta na kuhifadhiwa na kuyatumia baadaye kulingana na matakwa ya mtumiaji. Ndiyo
maana ukitaka kuandika barua katika kompyuta unafungua program inayohusika na kuanza
kuandika barua hiyo. Ukimaliza unaifunga program hiyo na siku nyingine au mtu mwingine
anaweza kuitumia.
Kuna aina kuu NNE za Kompyuta
Kompyuta hutofautiana Sana kulingana na kazi inayopaswa kufanya. Kompyuta inayotumika
katika lift za majengo si sawa na kompyuta inayotumika katika mahospitali kusaidia kutibu
wagonjwa. Kulingana na matumizi husika, kompyuta hutofautiana ukubwa, bei, uwezo wa kufanya
kazi na hata uendeshwaji wake.
Aina ya kwanza ya Kompyuta
Kompyuta aina ya kwanza ni zile ambazo mara nyingi watu wa kawaida huzimiliki majumbani
na maofisini na ndizo zilizo za bei ya chini, uwezo mdogo na umbo dogo zaidi kuliko aina
nyingine ya kompyuta. Kompyuta hizi hujulikana kama personal computers au PC kwa
kifupi. Ukitazama Kwa undani zaidi utagundua kuwa kompyuta hizi ni maalum kwa ajili ya
matumizi binafsi ya mtu au kwa ajili ya kuendeshea mitambo midogo midogo kwa faida ya maisha
ya kila siku ya binadamu. Kompyuta hizi hupatikana katika maumbo mbalimbali. Zipo desktop Na
tower computers ambazo hupatikana mara nyingi maofisini katika meza; notebook computers
ambayo hujulikana Sana Kama laptops; zipo palm tops (kompyuta za viganjani ambazo hujulikana
Sana Kama PDA-Personal Digita Assistant). Hizi ndizo kompyuta ambazo mara nyingi tunaziona
katika maduka na supermarkets zinazouza kompyuta. Tutakuwa Na sehemu kubwa ya kutazama
juu ya kompyuta aina hii huko mbele Kwa sababu ndizo zinazotumika Na kuonekana zaidi Kwa
sasa mionogni mwa watu wa kawaida.
Kompyuta aina ya personal
Aina ya pili ya Kompyuta
Aina ya pili ya kompyuta inajulikana kama miniframe computers. Aina hii ya kompyuta ina
uwezo, na ukubwa zaidi ya aina ya kwanza na ni ghali zaidi. Ni kompyuta ambazo
zimetengenezwa maalum Kwa ajili ya kufanyia kazi zinazohitaji nguvu kubwa na za haraka
zaidi. Mitambo mingi ya kuendeshea mawasiliano ya habari katika majengo makubwa huendeshwa
Kwa kutumia kompyuta hizi
Aina ya tatu ya Kompyuta
Aina ya tatu ya kompyuta ni zile zijulikanazo kama Mainframe computers. Hizi ni kompyuta
zenye uwezo mkubwa na zinazogharimu fedha nyingi. Hutumika katika utafiti katika
maabara za kisayansi katika sehemu maalum hasa katika taasisi za utaiti na katika vyuo
vikuu. Pia katika kuendesha mitambo ya kutafiti maswala ya hali ya hewa (weather forecast). Kwa
mfano, pale mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) makao makuu unaweza kukuta kompyuta
ya namna hii.
Aina ya NNE ya Kompyuta
Aina ya nne na ya mwisho ya kompyuta ni ile iitwayo super-computers. Hizi ni kompyuta
ambazo ni kubwa na zenye nguvu sana na ambazo huweza kugharimu mamilion ya dolla. Ni
kompyuta hizi ambazo hutumika katika kuendesha mitambo ya kinyukilia (nuclear control)
na urushaji wa maroket katika kufanya utafiti katika sayari za mbali (space exploration). Hizi
kompyuta zinahitaji watu wenye utaalam wa juu katika kuziendesha na kuzifanyia marekebisho
Kompyuta aina ya Supercomputer
Kompyuta aina ya Notebook ama Laptop
Kompyuta aina ya notebook ni kama gari dogo la kuendeshea mambo nyumbani. Kila kitu kuanzia
muonekano wa nje yaani hardware, mpaka katika matumizi ya nishati ya umeme kuendeshea
programs ni madogo. Kwa namna hii wataalam wa masuala ya umeme katika kompyuta ya aina hii
wamefanya kazi kubwa ya kupunguza matumizi ya umeme na mahitaji ya ukubwa katika sehemu
zote za kompyuta hii. Ukubwa wa kompyuta hii pamoja na matumizi ya umeme yanapunguzwa
kadiri inavyowezekana. Kwa mfano hard disks za notebook computer ni ndogo kuliko hard
disks za desktop computers na zinaweza kupachikwa katika upande mmoja wa system unit au
kuwekwa katika sehemu ya chini ya system unit
Katika nyakati hizi CPUs za notebook computer zijulikanazo Kama Mobile CPUs zina muundo
maalum unaozitofautisha na zile za zamani. Mobile CPU Ni aina maalum ya CPU kwa kompyuta
aina ya Notebook ama Laptop ambayo hubadilisha mwendokasi (wa kufafanua maelekezo) na
hivyo matumizi ya umeme kwa kadiri ya kupungua au kuongezeka kwa mahitaji ya kufafanua
(exection of instructions) maelekezo hayo. Kwa mfano CPU ya desktop kompyuta yenye uwezo wa
kufafanua maelekezo katika mwendokasi wa 1 GH (CPU speed) inatumia kati ya wati (watts) 75
mpaka 100 za umeme ilihali CPU aina ya Mobile ya Notebook kompyuta kwa mfano SpeedStep
CPU ambayo hutumia kiwango cha wati 34 za umeme wakati notebook kompyuta hii
imechomekwa katika waya ya kuingizia umeme. Hii husababisha kupunguka Kwa umeme ambao
CPU huhitaji na hivyo kusababisha kuzalishwa kwa kiwango kidogo cha joto ambalo husababisha
feni ya kupoza joto hilo kutumia umeme mdogo.
Feni ya CPU ya notebook kompyuta huwa haifanyi kazi muda wote Kama ilivyo Kwa feni za
kompyuta za aina nyingine. Feni hufanya kazi pale tu joto linapokuwa limezidi kiwango Fulani.
Kumbuka kwamba Notebook kompyuta huwa Na Betri inayoweza kutunza umeme Na hivyo
kukuwezesha wewe kuitumia bila kuichomeka kwenye soketi ya umeme. Ni Kama unavyoweza
kuingiza umeme kwenye simu ya mkononi Na inapokuwa umejaa unaenda zako ukitumia Na
unapokuwa umekwisha unarudi Na kujaza tena
Kompyuta aina ya laptop katika maumbo mbalimbali

Post a Comment