Muigizaji maarufu Tanzania Mzee Small, amefariki dunia. Chanzo cha taarifa hizi ni Mtoto wake wa kiume Mahmudu (Mongamba) ambae amenipigia simu sasa hivi muda ni saa 7 usiku.
Anasema Baba yake alipelekwa hospitali ya Muhimbili Jumamosi Tar 7 yani jana, muda wa saa mbili asubuhi baada ya kuzidiwa.
Ameeleza kwamba alishinda nae kutwa nzima ila ilivofika saa 4:09 usiku akafariki akiwa mikononi mwake.
Mzee small alikua anasumbuliwa na tatizo la kupooza kwa muda mrefu
Post a Comment