Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

JUSTIN BIEBER ATUHUMIWA KUTUMIA NENO LA KIBAGUZI

JUSTIN BIEBER ATUHUMIWA KUTUMIA NENO LA KIBAGUZI
Picha ya video inayomuonesha msanii Justin Bieber akitumia neno la kibaguzi dhidi ya watu weusi imepatikana na gazeti moja.
Picha hiyo iliyopatikana na gazeti la The Sun, ilipigwa mwaka 2011 wakati wakitengeneza filamu yake ya 'Never Say Never'.
Picha hiyo inamuonesha Bieber akiwa kwenye kochi na marafiki zake na kuuliza "Kwanini watu weusi wanaogopa misumeno?".
Mwimbaji huyo ambaye umri wake sasa ni miaka 20 anamalizia sentensi yake kwa kufanya mlio wa msumeno na kisha kutumia neno la kibaguzi mara tano.
Gazeti hilo linadai kuwa baadhi ya watu wa karibu wa Bieber wamekuwa wakijaribu kuficha picha hiyo ya video kuonekana hadharani.
Tovuti ya Newsbeat ya BBC ilijaribu kuwasiliana na mwimbaji huyo kwa simu na barua pepe, lakini hakuna jibu lolote lililopatikana hadi sasa.
Bieber amekuwa na mwaka wenye misukosuko.
Jaji wa mahakama moja mjini Florida aliahirisha kesi yake ya tuhuma za kuendesha gari akiwa amelewa, hadi mwezi Julai.
Mwimbaji huyo pia anakabiliwa na mashtaka ya kuendesha gari na leseni iliyopita muda wake na kugoma kukamatwa na polisi.
Bieber pia anakabiliwa na mashtaka nchini Canada ya kumshambulia mtu kwa kumpiga kichwani.
Pia, nyumba yake ilipekuliwa na polisi mwezi Januari, baada ya kutuhumiwa kusababisha hasara ya maelfu ya dola katika nyumba ya jirani yake baada ya kuishambulia kwa kurusha mayai.
JUSTIN BIEBER ATUHUMIWA KUTUMIA NENO LA KIBAGUZI Picha ya video inayomuonesha msanii Justin Bieber akitumia neno la kibaguzi dhidi ya watu weusi imepatikana na gazeti moja. Picha hiyo iliyopatikana na gazeti la The Sun, ilipigwa mwaka 2011 wakati wakitengeneza filamu yake ya 'Never Say Never'. Picha hiyo inamuonesha Bieber akiwa kwenye kochi na marafiki  zake na kuuliza "Kwanini watu weusi wanaogopa misumeno?". Mwimbaji huyo ambaye umri wake sasa ni miaka 20 anamalizia sentensi yake kwa kufanya mlio wa msumeno na kisha kutumia neno la kibaguzi mara tano. Gazeti hilo linadai kuwa baadhi ya watu wa karibu wa Bieber wamekuwa wakijaribu kuficha picha hiyo ya video kuonekana hadharani. Tovuti ya Newsbeat ya BBC ilijaribu kuwasiliana na mwimbaji huyo kwa simu na barua pepe, lakini hakuna jibu lolote lililopatikana hadi sasa. Bieber amekuwa na mwaka wenye misukosuko. Jaji wa mahakama moja mjini Florida aliahirisha kesi yake ya tuhuma za kuendesha gari akiwa amelewa, hadi mwezi Julai. Mwimbaji huyo pia anakabiliwa na mashtaka ya kuendesha gari na leseni iliyopita muda wake na kugoma kukamatwa na polisi. Bieber pia anakabiliwa na mashtaka nchini Canada ya kumshambulia mtu kwa kumpiga kichwani. Pia, nyumba yake ilipekuliwa na polisi mwezi Januari, baada ya kutuhumiwa kusababisha hasara  ya maelfu ya dola katika nyumba ya jirani yake baada ya kuishambulia kwa kurusha mayai.

Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana

Total Pageviews

Followers

Navigation-Menus (Do Not Edit Here!)

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.

www.CodeNirvana.in

Sponsor Ads close

Sponsor Ads


© Copyright T0T00
Back To Top