Hajavutiwa: Manuel Pellegrini ameipiga chini ofa ya kurithi mikoba ya Luiz Felipe Scolari .
KOCHA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amekataa ofa ya kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Brazil, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Chile.
Inaelezwa kuwa Pellegrini alifuatwa wakati wa mechi ya fainali ya kombe la dunia siku ya jumapili, saa 24 kabla ya Luiz Felipe Scolari kuachishwa kazi kutokana na matokeo mabaya ya Brazil katika mashindano hayo yaliyofanyika katika ardhi yake.
Brazil ilifungwa mabao 7-1 katika mchezo wa nusu fainali na Ujerumani na ikafungwa mabao 3-0 dhidi ya Uholanzi kwenye mechi ya kutafuta mshindi wa tatu.
Ingawa inasemekana kuwa Pellegrini amegoma kuingia katika makubaliano na shirikisho la soka nchini Brazil, amesisitiza kuwa anahitaji kuona miaka yake yake mitatu iliyosalia katika mkataba wake ndani ya dimba la Etihad.
Pellegrini na kikosi chake wapo katika mazoezi ya wiki moja, St Andrews nchini Scotland kabla ya kucheza mechi yao ya pili ya kujipima ubavu dhidi ya Hearts siku ya ijumaa.
Naye mkurugenzi wa michezo, Txiki Begiristain inasemekana anatakiwa, japokuwa haijawekwa wazi kama tayari ameshafuatwa na Brazil kwa mazungumzo.
Post a Comment