Mkali wa Bongo Flava Tanzania Diamond Platnumz amepewa nafasi ya kushirikiana na Mziiki kama Brand Partner. Msanii huyu ambaye amefanikiwa kushinda tuzo mbalimbali amekuwa wa kwanza kutia saini kama Brand Partner na tayari ni mmoja wa mamia ya wasanii pekee wa Afrika walio katika program ya muziki unaopendwa zaidi Afrika kupitia simu za kiganjani pamoja na kuwa mwakilishi wa bidhaa hiyo akiwakilisha nchi yake.
“Tunafurahi kwamba Diamond Platnumz kwa sasa ni Brand Partner wa Mziiki,” anasema Arun Nagar, Mkurugenzi Mtendaji wa Spice VAS Africa, watengenezaji wa Mziiki. “Kwa kushirikiana na msanii mwenye kiwango kama Diamond pamoja na mashabiki wake ni hatua nzuri kwa Mziiki. Ushirikiano kama huu unaonyesha dhamira yetu ili kuendelea kuhakikisha kwamba watumiaji wetu na muziki bora wa Afrika unawafikia pale walipo na tutaweza kufanya kazi karibu na Diamond na kupanua wigo wa wateja wetu na kuwapatia mashabiki wake zaidi ya kile walichotarajia. Nadhani pia ni ushahidi wa ukweli kwamba sisi tumechukua nafasi kubwa katika ulimwengu wa muziki streaming na wapenzi wa muziki wa Afrika wanapaswa kukumbuka hilo. ”Partnership between Bongo flava super star and music streaming app Mziiki. Diamond shakes hands with Arun Nagar CEO for Spice VAS Africa creators of Mziiki.
Post a Comment