Featured

    Featured Posts

    Social Icons

Loading...

NAHODHA WAYNE ROONEY AIOMBA RADHI TIMU KWA KADI NYEKUNDU!

>>FA KUMWADHIBU DIAFRA SAKHO KWA ‘KUMPIGA KICHWA’ LUKE SHAW?
WAYNE ROONEY ametoboa kuwa amewaomba radhi Wachezaji wenzake kwa kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Jumamosi huko Old Trafford wakati Manchester United inaifunga West Ham.ROONEY-KILIO
Rooney alipewa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 54 na Refa Lee Mason kwa kumchezea Rafu Stewart Downing na amesema hana mpango wa kukata Rufaa.
Kutokana na Kadi hiyo, Rooney atazikosa Mechi 3 za Ligi ambazo ni dhidi ya Everton, WBA na Chelsea na atarejea Uwanjani Novemba 2 kwenye Dabi ya Jiji la Manchester dhidi ya Man City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
WAYNE ROONEY – KADI NYEKUNDU:
-27 Sep 2014 - Man United 2 West Ham 1 (Ligi Kuu England)
-1 Julai2006 - England 0 Portugal 0 (Penati 1-3, Kombe la Dunia)
-7 Okt 2011 - England 2 Montenegro 2 (Euro 2012 Mchujo)
-14 Sep 2005 - Man United 0 Villarreal 0 (UEFA CHAMPIONZ LIGI)
-21 Machi 2009 - Man United 0 Fulham 2 (Ligi Kuu England)
-26 Des 2002 – Everton 1 Birmingham 1 (1-1, Ligi Kuu England)
++++++++++++++++++++++++++++++++++++++
Kuhusu Kadi hiyo, Bosi wa Man United, Louis van Gaal, alikiri kuwa ilistahili kwani alikosea jinsi ya kumsimamisha Downing aliekuwa akichanja mbuga .
Mwenyewe Rooney ameeleza: “Nilimwona Mchezaji wa West Ham akifanya kaunta ataki na mimi nilijaribu kuvunja hiyo lakini nilikosea namna ya kumzuia. Nimefarijika wenzangu walilinda Bao zetu na tumeshinda.”
Hata hivyo Mechi hiyo pia imekumbwa na tukio jingine la utata kwani Straika wa West Ham Diafra Sakho sasa anaweza kuadhibiwa na FA baada ya kudaiwa kumpiga Kichwa Beki wa Man United Luke Shaw wakati hawakuwa na Mpira na tukio hilo kutoonwa na Refa Lee Mason.
BPL-LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumatatu Septemba 29
2200 Stoke v Newcastle
Jumamosi Oktoba 4
1700 Hull v Crystal Palace
1700 Leicester v Burnley
1700 Liverpool v West Brom
1700 Sunderland v Stoke
1700 Swansea v Newcastle
1930 Aston Villa v Man City
Jumapili Oktoba 5
1400 Man United v Everton
1605 Chelsea v Arsenal
1605 Tottenham v Southampton
1815 West Ham v QPR
Get Free Email Updates to your Inbox!

Post a Comment

CodeNirvana

Total Pageviews

Followers

Navigation-Menus (Do Not Edit Here!)

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.

www.CodeNirvana.in

Sponsor Ads close

Sponsor Ads


© Copyright T0T00
Back To Top