SOMA ZAIDI:
JORDAN HENDERSON AMTETEA NAHODHA STEVEN GERRARD!
Jordan Henderson amemtetea Nahodha wake Steven Gerrard na kusisitiza kusakamwa kwake kwamba zama zake zimekwisha hakustahili.
Kufifia kwa Gerrard Msimu huu kumeelezwa ni moja ya sababu ya Liverpool kusuasua Msimu huu lakini Jumamosi walipocheza Dabi ya Merseyside na kutoka Sare 1-1 na Everton Gerrard ndie aliefunga Bao la Liverpool.
Henderson, ambae hucheza Kiungo pamoja na Gerrard, amesema: “Yeye bado ni mmoja wa Wachezaji bora wa Ligi hii. Timu nyingi zimekuwa zikiweka Mtu maalum kumkaba Uwanjani na hilo linaonyesha uzuri wake. Hastahili kulaumiwa!”
VINCENT KOMPANY AMTETEA MWENZAKE ELIAQUIM MANGALA!
Nahodha wa Manchester City Vincent Kompany amemtetea Eliaquim Mangala baada kuwa na majanga Jumamosi walipocheza Ugenini na Hull City na kushinda 4-2 kwenye Mechi ya Ligi lakini Bao zote za Hull zilitokana na makosa ya Mangala.
Huko KC Stadium, Bao la kwanza la Hull lilitokana na Mangala kujifunga mwenyewe na Bao la Pili ni kutokana na Penati pale Mangala alipomwangusha Fowadi na kuwafanya Hull watoke Bao 2-0 nyuma na kusawazisha na Gemu kuwa 2-2.
Hata hivyo Bao za Edin Dzeko na Frank Lampard ziliwapa City ushindi wa 4-2.
Sasa Kompany ameibuka na kusema: “Hiyo ni sehemu ya kuwa Difenda. Ikiwa Watoto wako wataamua kucheza Soka basi wawe Mastraika na hili halitawatokea!”
BPL-LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
**Saa za Bongo
Jumatatu Septemba 29
2200 Stoke v Newcastle
Jumamosi Oktoba 4
1700 Hull v Crystal Palace
1700 Leicester v Burnley
1700 Liverpool v West Brom
1700 Sunderland v Stoke
1700 Swansea v Newcastle
1930 Aston Villa v Man City
Jumapili Oktoba 5
1400 Man United v Everton
1605 Chelsea v Arsenal
1605 Tottenham v Southampton
1815 West Ham v QPR
Post a Comment