Chini ya Kanuni mpya za Ligi Kuu England Msimu huu, Watu ambao wanaamua Mchezaji atolewe nje ya Uwanja na kubadilishwa baada ya kupata dhoruba Kichwani ni Madaktari na si Meneja au Makocha wa Timu kama ilivyokuwa zamani.
Jumamosi, Harry Redknapp, Meneja wa QPR, alifadhaishwa wakati wa Mechi waliyofungwa na Southampton Bao 2-1 walipolazimishwa kumtoa na kumbadili Kiungo wao wa Brazil, Santo, baada ya Dakika 11 tu kufuatia kugongwa Kichwani.
Lakini Redknapp amesema baada ya muda Sandro alionekana yuko fiti kuendelea kucheza Mechi hiyo ingawa tayari alikuwa ameshabadilishwa na asingeweza kurudi tena Uwanjani.
Redknapp ameeleza: “Haiwezekani ungojee Dakika 10 au 15 ukiwa na Wachezaji 10 Uwanjani. Huwezi kuwapa Madaktari muda huo wote kumwangalia Mchezaji. Si vibaya kama wangeruhusu Wachezaji wa Akiba wa muda wakaingia kucheza wakati Mchezaji alieumia Kichwani wanamtafakari kama yuko fiti au la kuendelea. Madaktari wanakuwa katika wakati mgumu kuamua kwa haraka kama Mchezaji anaweza kuendelea au la!”
Aliongeza: “Kama Mchezaji kaumia vibaya ni wazi hawezi kuendelea na huwezi kumtaka aendelee kucheza kwani kama litatokea tatizo wote tutaathirika! Baadae tulimwona Sandro yuko fiti kabisa!”
Post a Comment