Msafara wa Dkt.Magufuli umepataja ajali Dodoma ukitokea Manyoni baada ya uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kuingia Manyoni Mjini (Manyoni Access Road) yenye urefu wa kilomita 4.8. Ajali hiyo ilihusisha gari la Mtendaji Mkuu wa Baraza la Taifa la Ujenzi na la Meneja wa Wakala wa Barabara Dododma.Waliojeruhiwa katika ajali hiyo ukiachilia Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi ni pamoja na Msajili wa CRB Eng. Boniface Muhegi, Mwenyekiti wa bodi ya CRB Eng.Consolatha Ngimbi na Meneja wa Wakala wa Barabara Dodoma Eng.Chimagu na mtu mwingine mmoja, hata hivyo majeruhi walikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma. Hata hivyo Dkt.Magufuli hakujeruhiwa kwenye msafara wake.
Ilivyokuwa: Dkt.Magufuli baada ya kuweka jiwe la msingi Manyoni, aliongozana na msafara wake akilekea Dodoma Mjini amabako alitakiwa kuhutubia na kufungua Taa za Barabarani Mjini Dodoma. Bahata mbaya msafara wake ukapata ajali. Hata hivyo Dkt.Magufuli aliweza kuendelea na ziara Mkoani Dodoma ambapo alihudhulia na kufanya ufunguzi wa Mataa ya barabarani mjini Dodoma akiambatana na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mkuu wa Wilaya, Wanajeshi pamoja na wananchi.
Uwekaji Jiwe la Msingi Barabara ya kuingia Manyoni Mjini: Dkt.Magufuli aliweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kuingia Manyoni Mjini (Manyoni Access Road) yenye urefu wa kilomita 4.8. Baadhi ya viongozi waliohudhrulia uwekaji wa jiwe la msingi ni pamoja na Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Mh.John Zefania Chiligati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mbunge wa zamani wa jimbo la Iramba Mashariki ndugu Mgana Izumbe Msindaiwa, Wenyeviti wa Bodi, wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara na wananchi.
Picha za Matukio:

Ufunguzi wa Mataa ya barabarani mjini Dodom,Dk.Magufuli,Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Mkuu wa Wilaya, Wanajeshi pamoja na wananchi.

Mataa ya Barabarani Mjini Dodoma, walioketi ni timu nzima ya ufunguzi ikiongozwa na Dkt.Magufuli

Uwekaji wa jiwe la Msingi barabara ya kwenda Manyoni Mjini, picha ya kumbukumbuku Dkt.Magufuli,Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mh.John Zefania Chiligati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mbunge wa zamani wa jimbo la Iramba Mashariki ndugu Mgana Izumbe Msindaiwa, Wenyeviti wa Bodi, wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara na wananchi.

Uzinduzi wa Barabar ya Kwenda Manyoni Mjini.

Dkt.Magufuli akikata utepe uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa barabara ya kuingia Manyoni Mjini wengine ni Mbunge wa jimbo la Manyoni Mashariki Mh.John Zefania Chiligati, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mkuu wa Wilaya, Mbunge wa zamani wa jimbo la Iramba Mashariki ndugu Mgana Izumbe Msindaiwa, Wenyeviti wa Bodi, wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi na Wafanyakazi wa Wakala wa Barabara.

Matukio ya Ajali ya gari la Mtendaji Mkuu wa Mtendaji Mkuu wa Baraza la Ujenzi, ambapo watu watano walijeruhiwa.

Post a Comment